Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Select Readings

802 mistari · 47 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mwanadamu hatambui thamani yake; haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

  2. Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’; bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’

  3. Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote, wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.

  4. Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri, kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.

  5. Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.

  6. Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu.

  7. Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.

  8. “Ni wapi basi hekima itokako? Ufahamu hukaa wapi?

  9. Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai, imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.

  10. Uharibifu na Mauti husema, ‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’

  11. Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,

  12. kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia na huona kila kitu chini ya mbingu.

  13. Alipofanyiza nguvu za upepo na kuyapima maji,

  14. alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia kwa ajili ya umeme wa radi,

  15. ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, akaithibitisha na kuihakikisha.

  16. Naye Mungu akamwambia mwanadamu, ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

  17. Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

  18. Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

  19. Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.

  20. Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

  21. Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

  22. Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia.

  23. Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure?

  24. Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

  25. Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”