Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Select Readings

802 mistari · 47 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.

  2. Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

  3. Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo.

  4. Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, hema lake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua ya angani.

  5. Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi.

  6. Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

  7. Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.

  8. Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.

  9. Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.

  10. Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.

  11. Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu.

  12. Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

  13. Zaburi ya Daudi. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.

  14. Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza,

  15. hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

  16. Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.

  17. Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika.

  18. Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

  19. Zaburi ya Daudi. Dunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake, ulimwengu, na wote waishio ndani yake,

  20. maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji.

  21. Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

  22. Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.

  23. Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

  24. Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao, wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

  25. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, inukeni enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia.