Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Select Readings: The majesty of God

19 mistari · 47 vipengele

Mistari kuhusu The majesty of God

  1. Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

  2. Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

  3. Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu.

  4. Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka.

  5. Mawingu yalimwaga maji, mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, mishale yako ikametameta huku na huko.

  6. Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, umeme wako wa radi ukaangaza dunia, nchi ikatetemeka na kutikisika.

  7. Njia yako ilipita baharini, mapito yako kwenye maji makuu, ingawa nyayo zako hazikuonekana.

  8. Uliongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Mose na Aroni.

  9. Mungu alitoka Temani, yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. Utukufu wake ulifunika mbingu, na sifa zake zikaifunika dunia.

  10. Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo; mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, ambako nguvu zake zilifichwa.

  11. Tauni ilimtangulia; maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.

  12. Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.

  13. Niliona watu wa Kushani katika dhiki, na makazi ya Midiani katika maumivu makali.

  14. Ee Bwana, uliikasirikia mito? Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito? Je, ulighadhibikia bahari ulipoendesha farasi wako na magari yako ya ushindi?

  15. Uliufunua upinde wako na kuita mishale mingi. Uliigawa dunia kwa mito;

  16. milima ilikuona ikatetemeka. Mafuriko ya maji yakapita huko; vilindi vilinguruma na kuinua mawimbi yake juu.

  17. Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.

  18. Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa.

  19. Ulikuja kuwaokoa watu wako, kumwokoa uliyemtia mafuta. Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, ukamvua toka kichwani hadi wayo.