Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Select Readings

802 mistari · 47 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

  2. Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

  3. Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu.

  4. Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka.

  5. Mawingu yalimwaga maji, mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, mishale yako ikametameta huku na huko.

  6. Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, umeme wako wa radi ukaangaza dunia, nchi ikatetemeka na kutikisika.

  7. Njia yako ilipita baharini, mapito yako kwenye maji makuu, ingawa nyayo zako hazikuonekana.

  8. Uliongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Mose na Aroni.

  9. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini!

  10. Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za Bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai.

  11. Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu.

  12. Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.

  13. Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.

  14. Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.

  15. Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni.

  16. Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.

  17. Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.

  18. Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu.

  19. Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.

  20. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.

  21. Zaburi. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu.

  22. Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.

  23. Ameukumbuka upendo wake na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.

  24. Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

  25. mwimbieni Bwana kwa kinubi, kwa kinubi na sauti za kuimba,