Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Animals

136 mistari · 25 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Unaleta giza, kunakuwa usiku, wanyama wote wa mwituni huzurura.

  2. Simba hunguruma kwa mawindo yao, na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.

  3. Jua huchomoza, nao huondoka, hurudi na kulala katika mapango yao.

  4. Kisha mwanadamu huenda kazini mwake, katika kazi yake mpaka jioni.

  5. Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako.

  6. Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.

  7. Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima!

  8. Kwa maana yeye hana msimamizi, wala mwangalizi, au mtawala,

  9. lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

  10. Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.

  11. Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba.

  12. Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.

  13. Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme.

  14. Pia nikafikiri, “Kuhusu wanadamu, Mungu huwajaribu ili wajione kwamba wao ni kama wanyama.

  15. Hatima ya mwanadamu ni kama ile ya wanyama; wote wana mwisho unaofanana: Jinsi anavyokufa mnyama, ndivyo anavyokufa mwanadamu. Wote wana pumzi inayofanana; mwanadamu hana cha zaidi kuliko mnyama. Kila kitu ni ubatili.

  16. Wote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi.

  17. Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?”

  18. Lakini viumbe wa jangwani watalala huko, mbweha watajaza nyumba zake, bundi wataishi humo nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.

  19. Fisi watalia ndani ya ngome zake, mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari. Wakati wake umewadia, na siku zake hazitaongezwa.

  20. “Au kama nikipeleka tauni katika nchi hiyo na kumwaga ghadhabu yangu juu yake kwa njia ya kumwaga damu, kuua watu wake na wanyama wao,

  21. hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.

  22. “Kwa maana hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao!

  23. Jinsi gani ngʼombe wanavyolia! Makundi ya mifugo yanahangaika kwa sababu hawana malisho; hata makundi ya kondoo yanateseka.

  24. Kwako, Ee Bwana, naita, kwa kuwa moto umeteketeza malisho ya mbugani na miali ya moto imeunguza miti yote shambani.

  25. Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku; vijito vya maji vimekauka, na moto umeteketeza malisho yote ya mbugani.