Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Animals: Clean and unclean

26 mistari · 25 vipengele

Mistari kuhusu Clean and unclean

Chuja kwa kitabu
  1. Msile kitu chochote ambacho ni machukizo.

  2. Hawa ndio wanyama mtakaokula: ngʼombe, kondoo, mbuzi,

  3. kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani.

  4. Mnaweza kumla mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua.

  5. Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.

  6. Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.

  7. Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula yeyote aliye na mapezi na magamba.

  8. Lakini chochote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.

  9. Mnaweza kula ndege yeyote aliye safi.

  10. Lakini wafuatao msiwale: tai, furukombe, kipungu,

  11. kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yoyote,

  12. kunguru wa aina yoyote,

  13. mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote,

  14. bundi, mumbi, bundi mkubwa,

  15. mwari, nderi, mnandi,

  16. korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.

  17. Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.

  18. Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

  19. Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne.

  20. Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani.

  21. Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”

  22. Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”

  23. Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”

  24. Wao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, ambavyo Mungu aliviumba ili vipokewe kwa shukrani na wale wanaoamini na kuijua kweli.

  25. Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani,