Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Animals: Habits of

10 mistari · 25 vipengele

Mistari kuhusu Habits of

  1. “Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, au ndege wa angani, nao watawaambia;

  2. au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.

  3. Unaleta giza, kunakuwa usiku, wanyama wote wa mwituni huzurura.

  4. Simba hunguruma kwa mawindo yao, na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.

  5. Jua huchomoza, nao huondoka, hurudi na kulala katika mapango yao.

  6. Kisha mwanadamu huenda kazini mwake, katika kazi yake mpaka jioni.

  7. Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako.

  8. Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.

  9. Lakini viumbe wa jangwani watalala huko, mbweha watajaza nyumba zake, bundi wataishi humo nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.

  10. Fisi watalia ndani ya ngome zake, mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari. Wakati wake umewadia, na siku zake hazitaongezwa.