Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Samweli 5:16takriban 1048 KK

    Elishama, Eliada na Elifeleti.

  2. 2 Samweli 5:17takriban 1048 KK

    Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome.

  3. 2 Samweli 5:18takriban 1048 KK

    Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai,

  4. 2 Samweli 5:19takriban 1048 KK

    kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.”

  5. 2 Samweli 5:20takriban 1048 KK

    Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.

  6. 2 Samweli 5:21takriban 1048 KK

    Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua.

  7. 2 Samweli 5:22takriban 1048 KK

    Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai.

  8. 2 Samweli 5:23takriban 1048 KK

    Kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi.

  9. 2 Samweli 5:24takriban 1048 KK

    Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa Bwana ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.”

  10. 2 Samweli 5:25takriban 1048 KK

    Basi Daudi akafanya kama Bwana alivyomwagiza, naye akawaangusha Wafilisti njia yote kuanzia Geba hadi Gezeri.

  11. 2 Samweli 6:1takriban 1042 KK

    Tena Daudi akakusanya watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa.

  12. 2 Samweli 6:2takriban 1042 KK

    Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku.

  13. 2 Samweli 6:3takriban 1042 KK

    Wakaweka hilo Sanduku la Mungu juu ya gari jipya la kukokotwa na kulileta kutoka nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wana wa Abinadabu, walikuwa wakiongoza hilo gari jipya la kukokotwa

  14. 2 Samweli 6:4takriban 1042 KK

    likiwa na Sanduku la Mungu juu yake, naye Ahio alikuwa anatembea akiwa mbele yake.

  15. 2 Samweli 6:5takriban 1042 KK

    Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi.

  16. 2 Samweli 6:6takriban 1042 KK

    Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Nakoni, Uza akanyoosha mkono na kulishika Sanduku la Mungu kwa sababu maksai walijikwaa.

  17. 2 Samweli 6:7takriban 1042 KK

    Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza kwa sababu ya kitendo chake cha kukosa heshima, kwa hiyo Mungu akampiga akafia papo hapo kando ya Sanduku la Mungu.

  18. 2 Samweli 6:8takriban 1042 KK

    Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya Bwana ilifurika dhidi ya Uza, hivyo hadi leo mahali hapo panaitwa Peres-Uza.

  19. 2 Samweli 6:9takriban 1042 KK

    Daudi akamwogopa Bwana siku ile, akasema, “Ni jinsi gani Sanduku la Bwana litakavyoweza kunijia?”

  20. 2 Samweli 6:10takriban 1042 KK

    Hakuwa radhi kulichukua Sanduku la Bwana kwake katika Mji wa Daudi. Badala yake akalipeleka kwenye nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti.

  21. 2 Samweli 6:11takriban 1042 KK

    Sanduku la Bwana likabaki katika nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti, kwa miezi mitatu, naye Bwana akambariki pamoja na nyumba yake yote.

  22. 2 Samweli 6:12takriban 1042 KK

    Kisha Mfalme Daudi akaambiwa, “Bwana ameibariki nyumba ya Obed-Edomu pamoja na kila alicho nacho, kwa sababu ya Sanduku la Mungu.” Basi Daudi akateremka na kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka nyumba ya Obed-Edomu hadi Mji wa Daudi kwa shangwe.

  23. 2 Samweli 6:13takriban 1042 KK

    Wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Bwana walipokuwa wametembea hatua sita, Daudi alitoa dhabihu fahali na ndama aliyenoneshwa.

  24. 2 Samweli 6:14takriban 1042 KK

    Daudi, akiwa amevaa kisibau cha kitani, alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote,

  25. 2 Samweli 6:15takriban 1042 KK

    wakati yeye na nyumba yote ya Israeli walipopandisha Sanduku la Bwana kwa shangwe na sauti za tarumbeta.