circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Marko 14:66takriban 33 BK
Petro alipokuwa bado yuko chini kwenye ua wa jumba la kifalme, tazama akaja mmoja wa watumishi wa kike wa kuhani mkuu.
- Marko 14:67takriban 33 BK
Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”
- Marko 14:68takriban 33 BK
Lakini Petro akakana, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema.” Naye akaondoka kuelekea kwenye njia ya kuingilia.
- Marko 14:69takriban 33 BK
Yule mtumishi wa kike alipomwona mahali pale, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama hapo, “Huyu mtu ni mmoja wao.”
- Marko 14:70takriban 33 BK
Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo karibu na Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!”
- Marko 14:71takriban 33 BK
Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui huyu mtu mnayesema habari zake!”
- Marko 14:72takriban 33 BK
Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.
- Marko 15:1takriban 33 BK
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.
- Marko 15:2takriban 33 BK
Pilato akamuuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.”
- Marko 15:3takriban 33 BK
Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi.
- Marko 15:4takriban 33 BK
Pilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.”
- Marko 15:5takriban 33 BK
Lakini Yesu hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa.
- Marko 15:6takriban 33 BK
Ilikuwa desturi wakati wa Sikukuu ya Pasaka kumfungulia mfungwa yeyote ambaye watu wangemtaka.
- Marko 15:7takriban 33 BK
Wakati huo, mtu aliyeitwa Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wametekeleza uuaji wakati wa maasi.
- Marko 15:8takriban 33 BK
Ule umati wa watu ukamjia Pilato na kumwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi yake.
- Marko 15:9takriban 33 BK
Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie huyu Mfalme wa Wayahudi?”
- Marko 15:10takriban 33 BK
Kwa maana yeye alitambua kuwa viongozi wa makuhani walikuwa wamemtia Yesu mikononi mwake kwa ajili ya wivu.
- Marko 15:11takriban 33 BK
Lakini viongozi wa makuhani wakauchochea ule umati wa watu wamwombe awafungulie Baraba badala yake.
- Marko 15:12takriban 33 BK
Pilato akawauliza tena, “Basi mnataka nifanye nini na huyu mtu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?”
- Marko 15:13takriban 33 BK
Wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe!”
- Marko 15:14takriban 33 BK
Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, wakisema, “Msulubishe!”
- Marko 15:15takriban 33 BK
Pilato, akitaka kuuridhisha ule umati wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.
- Marko 15:16takriban 33 BK
Askari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
- Marko 15:17takriban 33 BK
Wakamvalisha Yesu joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani.
- Marko 15:18takriban 33 BK
Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!”