Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Zekaria 9:15takriban 487 KK

    na Bwana Mwenye Nguvu Zote atawalinda. Wataangamiza na kushinda kwa mawe ya kutupa kwa kombeo. Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo; watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia kwenye pembe za madhabahu.

  2. Zekaria 9:16takriban 487 KK

    Bwana Mungu wao atawaokoa siku hiyo kama kundi la watu wake. Watangʼara katika nchi yake kama vito vya thamani kwenye taji.

  3. Zekaria 9:17takriban 487 KK

    Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! Nafaka itawastawisha vijana wanaume, nayo divai mpya vijana wanawake.

  4. Zekaria 10:1takriban 487 KK

    Mwombeni Bwana mvua wakati wa vuli; ndiye Bwana atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

  5. Zekaria 10:2takriban 487 KK

    Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo; husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioonewa kwa kukosa mchungaji.

  6. Zekaria 10:3takriban 487 KK

    “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi mwenye kiburi akiwa vitani.

  7. Zekaria 10:4takriban 487 KK

    Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni, kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema, kutoka kwake utatoka upinde wa vita, kutoka kwake atatoka kila mtawala.

  8. Zekaria 10:5takriban 487 KK

    Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa wanaokanyaga barabara za matope wakati wa vita. Kwa sababu Bwana yu pamoja nao, watapigana na kuwashinda wapanda farasi.

  9. Zekaria 10:6takriban 487 KK

    “Nitaiimarisha nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yosefu. Nitawarejesha kwa sababu nina huruma juu yao. Watakuwa kama watu ambao sijawahi kuwakataa kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wao, nami nitawajibu.

  10. Zekaria 10:7takriban 487 KK

    Waefraimu watakuwa kama mashujaa, mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai. Watoto wao wataona na kufurahi, mioyo yao itashangilia katika Bwana.

  11. Zekaria 10:8takriban 487 KK

    Nitawaashiria na kuwakusanya ndani. Hakika nitawakomboa, nao watakuwa wengi kama walivyokuwa mwanzoni.

  12. Zekaria 10:9takriban 487 KK

    Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa, hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali watanikumbuka mimi. Wao na watoto wao watanusurika katika hatari nao watarudi.

  13. Zekaria 10:10takriban 487 KK

    Nitawarudisha kutoka Misri na kuwakusanya toka Ashuru. Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni, na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.

  14. Zekaria 10:11takriban 487 KK

    Watapita katika bahari ya mateso; bahari iliyochafuka itatulizwa na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitashushwa, nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.

  15. Zekaria 10:12takriban 487 KK

    Nitawaimarisha katika Bwana, na katika jina lake watatembea,” asema Bwana.

  16. Zekaria 11:1takriban 487 KK

    Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mierezi yako!

  17. Zekaria 11:2takriban 487 KK

    Piga yowe, ee mti wa msunobari, kwa kuwa mwerezi umeanguka; miti ya fahari imeharibiwa! Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, msitu mnene umefyekwa!

  18. Zekaria 11:3takriban 487 KK

    Sikiliza yowe la wachungaji; malisho yao manono yameangamizwa! Sikia ngurumo za simba; kichaka kilichostawi sana cha Yordani kimeharibiwa!

  19. Zekaria 11:4takriban 487 KK

    Hili ndilo asemalo Bwana Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa.

  20. Zekaria 11:5takriban 487 KK

    Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Bwana asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.

  21. Zekaria 11:6takriban 487 KK

    Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema Bwana. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”

  22. Zekaria 11:7takriban 487 KK

    Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi.

  23. Zekaria 11:8takriban 487 KK

    Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu. Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao,

  24. Zekaria 11:9takriban 487 KK

    nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.”

  25. Zekaria 11:10takriban 487 KK

    Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote.