- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 970–930 BC
Solomon & The Temple
Solomon builds the great Temple in Jerusalem and rules with unprecedented wisdom and wealth before foreign gods divide his heart.
Mistari ya kipindi hiki
- 1 Wafalme 3:27takriban 1014 KK
Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: “Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimuue; ndiye mama yake.”
- 1 Wafalme 3:28takriban 1014 KK
Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.
- 1 Wafalme 4:1takriban 1014 KK
Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote.
- 1 Wafalme 4:2takriban 1014 KK
Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu: Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki;
- 1 Wafalme 4:3takriban 1014 KK
Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani;
- 1 Wafalme 4:4takriban 1014 KK
Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi; Sadoki na Abiathari: makuhani;
- 1 Wafalme 4:5takriban 1014 KK
Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya; Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme;
- 1 Wafalme 4:6takriban 1014 KK
Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme; Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha.
- 1 Wafalme 4:7takriban 1014 KK
Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.
- 1 Wafalme 4:8takriban 1014 KK
Majina yao ni haya: Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu;
- 1 Wafalme 4:9takriban 1014 KK
Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani;
- 1 Wafalme 4:10takriban 1014 KK
Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake);
- 1 Wafalme 4:11takriban 1014 KK
Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni);
- 1 Wafalme 4:12takriban 1014 KK
Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu;
- 1 Wafalme 4:13takriban 1014 KK
Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba);
- 1 Wafalme 4:14takriban 1014 KK
Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu;
- 1 Wafalme 4:15takriban 1014 KK
Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni);
- 1 Wafalme 4:16takriban 1014 KK
Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi;
- 1 Wafalme 4:17takriban 1014 KK
Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;
- 1 Wafalme 4:18takriban 1014 KK
Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;
- 1 Wafalme 4:19takriban 1014 KK
Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo.
- 1 Wafalme 4:20takriban 1014 KK
Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi.
- 1 Wafalme 4:21takriban 1014 KK
Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.
- 1 Wafalme 4:22takriban 1014 KK
Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini za unga laini, kori sitini za unga wa kawaida.
- 1 Wafalme 4:23takriban 1014 KK
Ngʼombe kumi wa zizini, ngʼombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana.