Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waebrania 10:23takriban 64 BK

    Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumbayumba, kwa maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.

  2. Waebrania 10:24takriban 64 BK

    Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema.

  3. Waebrania 10:25takriban 64 BK

    Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi, bali tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia.

  4. Waebrania 10:26takriban 64 BK

    Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi.

  5. Waebrania 10:27takriban 64 BK

    Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao, utakaowaangamiza adui za Mungu.

  6. Waebrania 10:28takriban 64 BK

    Yeyote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu.

  7. Waebrania 10:29takriban 64 BK

    Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema?

  8. Waebrania 10:30takriban 64 BK

    Kwa kuwa tunamjua yeye aliyesema, “Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.” Tena asema, “Bwana atawahukumu watu wake.”

  9. Waebrania 10:31takriban 64 BK

    Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai.

  10. Waebrania 10:32takriban 64 BK

    Kumbukeni siku zile za kwanza, ambazo mkiisha kutiwa nuru mlistahimili mashindano makali ya maumivu.

  11. Waebrania 10:33takriban 64 BK

    Wakati mwingine mlitukanwa na kuteswa hadharani; wakati mwingine mlikuwa radhi kuungana na wale waliofanyiwa hivyo.

  12. Waebrania 10:34takriban 64 BK

    Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyangʼanywa mali zenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.

  13. Waebrania 10:35takriban 64 BK

    Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kubwa mno.

  14. Waebrania 10:36takriban 64 BK

    Inawapasa kuvumilia ili mkiisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi.

  15. Waebrania 10:37takriban 64 BK

    Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu, “Yeye ajaye atakuja wala hatakawia.

  16. Waebrania 10:38takriban 64 BK

    Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Naye kama akisitasita, sina furaha naye.”

  17. Waebrania 10:39takriban 64 BK

    Lakini sisi hatumo miongoni mwa hao wanaositasita na kuangamia, bali tuko miongoni mwa hao wenye imani na hivyo tunaokolewa.

  18. Waebrania 11:1takriban 64 BK

    Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, na udhahiri wa mambo yasiyoonekana.

  19. Waebrania 11:2takriban 64 BK

    Maana baba zetu wa kale walipongezwa kwa haya.

  20. Waebrania 11:3takriban 64 BK

    Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vyote vinavyoonekana havikuumbwa kutoka kwa vitu vinavyoonekana.

  21. Waebrania 11:4takriban 64 BK

    Kwa imani Abeli alimtolea Mungu dhabihu bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alishuhudiwa kuwa mwenye haki, Mungu mwenyewe akazishuhudia sadaka zake. Kwa imani bado ananena ingawa amekufa.

  22. Waebrania 11:5takriban 64 BK

    Kwa imani Enoki alitwaliwa kutoka maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti. Hakuonekana, kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Kwa kuwa kabla hajatwaliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu.

  23. Waebrania 11:6takriban 64 BK

    Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.

  24. Waebrania 11:7takriban 64 BK

    Kwa imani, Noa alipoonywa na Mungu kuhusu mambo ambayo hayajaonekana bado, kwa kumcha Mungu alitengeneza safina ili kuokoa jamaa yake. Kwa imani yake aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

  25. Waebrania 11:8takriban 64 BK

    Kwa imani Abrahamu, alipoitwa aende mahali ambapo Mungu angempa baadaye kuwa urithi, alitii na akaenda, ingawa hakujua anakokwenda.