Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waebrania 9:26takriban 64 BK

    Ingekuwa hivyo, ingempasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu.

  2. Waebrania 9:27takriban 64 BK

    Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu,

  3. Waebrania 9:28takriban 64 BK

    vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.

  4. Waebrania 10:1takriban 64 BK

    Sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.

  5. Waebrania 10:2takriban 64 BK

    Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi.

  6. Waebrania 10:3takriban 64 BK

    Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka,

  7. Waebrania 10:4takriban 64 BK

    kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

  8. Waebrania 10:5takriban 64 BK

    Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani, alisema: “Dhabihu na sadaka hukuzitaka, bali mwili uliniandalia;

  9. Waebrania 10:6takriban 64 BK

    sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukupendezwa nazo.

  10. Waebrania 10:7takriban 64 BK

    Ndipo niliposema, ‘Mimi hapa, nimekuja, imeandikwa kunihusu katika kitabu: Nimekuja kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu.’ ”

  11. Waebrania 10:8takriban 64 BK

    Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe).

  12. Waebrania 10:9takriban 64 BK

    Kisha akasema “Mimi hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi yako.” Aondoa lile Agano la kwanza ili kuimarisha la pili.

  13. Waebrania 10:10takriban 64 BK

    Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.

  14. Waebrania 10:11takriban 64 BK

    Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi.

  15. Waebrania 10:12takriban 64 BK

    Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu.

  16. Waebrania 10:13takriban 64 BK

    Tangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake,

  17. Waebrania 10:14takriban 64 BK

    kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.

  18. Waebrania 10:15takriban 64 BK

    Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema:

  19. Waebrania 10:16takriban 64 BK

    “Hili ndilo Agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.”

  20. Waebrania 10:17takriban 64 BK

    Kisha aongeza kusema: “Dhambi zao na kutokutii kwao sitakumbuka tena.”

  21. Waebrania 10:18takriban 64 BK

    Basi haya yakiisha kusamehewa, hakuna tena dhabihu yoyote inayotolewa kwa ajili ya dhambi.

  22. Waebrania 10:19takriban 64 BK

    Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu,

  23. Waebrania 10:20takriban 64 BK

    kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kwa ajili yetu kupitia kwenye lile pazia, yaani, mwili wake,

  24. Waebrania 10:21takriban 64 BK

    basi kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu juu ya nyumba ya Mungu,

  25. Waebrania 10:22takriban 64 BK

    sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.