Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Yohana 3:2takriban 90 BK

    Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo.

  2. 1 Yohana 3:3takriban 90 BK

    Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.

  3. 1 Yohana 3:4takriban 90 BK

    Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi.

  4. 1 Yohana 3:5takriban 90 BK

    Lakini mwajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi, wala ndani yake hamna dhambi.

  5. 1 Yohana 3:6takriban 90 BK

    Kila mtu akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu atendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua.

  6. 1 Yohana 3:7takriban 90 BK

    Watoto wapendwa, mtu yeyote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki.

  7. 1 Yohana 3:8takriban 90 BK

    Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili aziangamize kazi za ibilisi.

  8. 1 Yohana 3:9takriban 90 BK

    Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.

  9. 1 Yohana 3:10takriban 90 BK

    Kwa jinsi hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na pia watoto wa ibilisi. Yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

  10. 1 Yohana 3:11takriban 90 BK

    Hili ndilo neno mlilolisikia tangu mwanzo: Kwamba imetupasa tupendane sisi kwa sisi.

  11. 1 Yohana 3:12takriban 90 BK

    Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu akamuua ndugu yake. Basi kwa nini alimuua? Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

  12. 1 Yohana 3:13takriban 90 BK

    Ndugu zangu, ninyi msistaajabu kama ulimwengu ukiwachukia.

  13. 1 Yohana 3:14takriban 90 BK

    Sisi tunajua ya kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini.

  14. 1 Yohana 3:15takriban 90 BK

    Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.

  15. 1 Yohana 3:16takriban 90 BK

    Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.

  16. 1 Yohana 3:17takriban 90 BK

    Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo?

  17. 1 Yohana 3:18takriban 90 BK

    Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.

  18. 1 Yohana 3:19takriban 90 BK

    Basi hivi ndivyo tutakavyoweza kujua ya kuwa sisi tu wa kweli na hivyo twaithibitisha mioyo yetu mbele za Mungu

  19. 1 Yohana 3:20takriban 90 BK

    kila mara mioyo yetu inapotuhukumu. Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu, naye anajua kila kitu.

  20. 1 Yohana 3:21takriban 90 BK

    Wapendwa, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri mbele za Mungu,

  21. 1 Yohana 3:22takriban 90 BK

    lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza.

  22. 1 Yohana 3:23takriban 90 BK

    Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru.

  23. 1 Yohana 3:24takriban 90 BK

    Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule aliyetupa.

  24. 1 Yohana 4:1takriban 90 BK

    Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni.

  25. 1 Yohana 4:2takriban 90 BK

    Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu.