Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Yohana 4:3takriban 90 BK

    Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.

  2. 1 Yohana 4:4takriban 90 BK

    Watoto wapendwa, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.

  3. 1 Yohana 4:5takriban 90 BK

    Wao wanatokana na ulimwengu na kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo ulimwengu huwasikiliza.

  4. 1 Yohana 4:6takriban 90 BK

    Sisi twatokana na Mungu na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.

  5. 1 Yohana 4:7takriban 90 BK

    Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.

  6. 1 Yohana 4:8takriban 90 BK

    Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo.

  7. 1 Yohana 4:9takriban 90 BK

    Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake.

  8. 1 Yohana 4:10takriban 90 BK

    Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.

  9. 1 Yohana 4:11takriban 90 BK

    Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana.

  10. 1 Yohana 4:12takriban 90 BK

    Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.

  11. 1 Yohana 4:13takriban 90 BK

    Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa sisi sehemu ya Roho wake.

  12. 1 Yohana 4:14takriban 90 BK

    Nasi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanawe ili awe Mwokozi wa ulimwengu.

  13. 1 Yohana 4:15takriban 90 BK

    Kila akiriye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, basi Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.

  14. 1 Yohana 4:16takriban 90 BK

    Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu. Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.

  15. 1 Yohana 4:17takriban 90 BK

    Kwa njia hii, pendo hukamilishwa miongoni mwetu ili tupate kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu, kwa sababu kama alivyo ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu.

  16. 1 Yohana 4:18takriban 90 BK

    Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo.

  17. 1 Yohana 4:19takriban 90 BK

    Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

  18. 1 Yohana 4:20takriban 90 BK

    Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona?

  19. 1 Yohana 4:21takriban 90 BK

    Naye ametupa amri hii: Yeyote anayempenda Mungu lazima pia ampende ndugu yake.

  20. 1 Yohana 5:1takriban 90 BK

    Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye.

  21. 1 Yohana 5:2takriban 90 BK

    Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake.

  22. 1 Yohana 5:3takriban 90 BK

    Huku ndiko kumpenda Mungu, yaani, kuzitii amri zake. Nazo amri zake si nzito.

  23. 1 Yohana 5:4takriban 90 BK

    Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.

  24. 1 Yohana 5:5takriban 90 BK

    Ni nani yule aushindaye ulimwengu? Ni yule tu aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

  25. 1 Yohana 5:6takriban 90 BK

    Huyu ndiye alikuja kwa maji na damu, yaani, Yesu Kristo. Hakuja kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.