Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?

  2. Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.

  3. Mwanangu, mche Bwana na mfalme, wala usijiunge na waasi,

  4. Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo.

  5. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake, naye Bwana atakupa thawabu.

  6. Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani.

  7. Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.

  8. Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa.

  9. Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.

  10. Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.

  11. Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.

  12. Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.

  13. Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!

  14. “Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.

  15. Usiongeze kwenye maneno yake, ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.

  16. “Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana; usininyime kabla sijafa:

  17. Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘Bwana ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.

  18. Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi, bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa.

  19. Nilitumia muda wangu wote kujifunza na kuvumbua kwa hekima yote yanayofanyika chini ya mbingu. Jinsi gani Mungu ameweka mzigo mzito juu ya wanadamu!

  20. Hakuna kitu bora anachoweza kufanya mtu zaidi ya kula na kunywa na kuridhika katika kazi yake. Hili nalo pia, ninaona, latokana na mkono wa Mungu,

  21. Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

  22. Nimeona mzigo Mungu alioweka juu ya wanadamu.

  23. Amefanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Pia ameiweka hiyo milele katika mioyo ya wanadamu, wala hawawezi kutambua kwa kina yale ambayo Mungu amefanya tangu mwanzo hadi mwisho.

  24. Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.

  25. Ninajua kwamba kila kitu anachokifanya Mungu kitadumu milele, hakuna kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa. Mungu hufanya hivyo ili watu wamche yeye.