Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.

  2. Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.

  3. Macho ya Bwana yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema.

  4. Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu.

  5. Bwana huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.

  6. Mauti na Uharibifu viko wazi mbele za Bwana: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu!

  7. Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.

  8. Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

  9. Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye.

  10. Bwana yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki.

  11. Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

  12. Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

  13. Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na Bwana.

  14. Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa.

  15. Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi.

  16. Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.

  17. Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.

  18. Njia za mtu zinapompendeza Bwana, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.

  19. Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.

  20. Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.

  21. Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana.

  22. Kura hupigwa kwa siri, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.

  23. Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali Bwana huujaribu moyo.

  24. Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Bwana huwachukia sana wote wawili.

  25. Jina la Bwana ni ngome imara, wenye haki huikimbilia na kuwa salama.