Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa Bwana.

  2. Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana.

  3. Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.

  4. Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, naye atamtuza kwa aliyotenda.

  5. Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu, lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.

  6. Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima, kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, bila kuguswa na shida.

  7. Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, Bwana huchukia vyote viwili.

  8. Masikio yasikiayo na macho yaonayo, Bwana ndiye alivifanya vyote viwili.

  9. Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!” Mngojee Bwana, naye atakuokoa.

  10. Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu, nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.

  11. Hatua za mtu huongozwa na Bwana. Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?

  12. Taa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani.

  13. Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana; huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo.

  14. Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali Bwana huupima moyo.

  15. Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.

  16. Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu, naye atawaangamiza waovu.

  17. Hakuna hekima, wala akili, wala mpango unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.

  18. Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Bwana.

  19. Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: Bwana ni Muumba wao wote.

  20. Unyenyekevu na kumcha Bwana huleta utajiri, heshima na uzima.

  21. Macho ya Bwana hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.

  22. Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu; yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana atatumbukia ndani yake.

  23. Ili tumaini lako liwe katika Bwana, hata wewe, ninakufundisha leo.

  24. kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao naye atawateka wao waliowateka.

  25. Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.