Skip to content
2 Samweli 23:13-39

2 Samweli 23:13-39

13
Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.
14
Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu.
15
Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu!”
16
Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana.
17
Akasema, “Iwe mbali nami, Ee Bwana, kufanya kitu hiki. Je, hii si damu ya watu ambao walikwenda kwa kuhatarisha maisha yao?” Naye Daudi hakuyanywa. Haya yalifanywa na hao mashujaa watatu.
18
Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.
19
Je, hakupata heshima kubwa zaidi kuliko hao Watatu? Alikuwa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.
20
Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.
21
Pia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe.
22
Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.
23
Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu. Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.
24
Miongoni mwa wale Thelathini walikuwepo: Asaheli ndugu wa Yoabu; Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu;
25
Shama, Mharodi; Elika, Mharodi;
26
Helesi, Mpalti; Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa;
27
Abiezeri kutoka Anathothi; Mebunai, Mhushathi;
28
Salmoni, Mwahohi; Maharai, Mnetofathi;
29
Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi; Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini;
30
Benaya Mpirathoni; Hidai kutoka mabonde ya Gaashi;
31
Abi-Alboni, Mwaribathi; Azmawethi, Mbarhumi;
32
Eliaba, Mshaalboni; wana wa Yasheni; Yonathani
33
mwana wa Shama, Mharari; Ahiamu mwana wa Sharari, Mharari;
34
Elifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaakathi; Eliamu mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;
35
Hezro, Mkarmeli; Paarai, Mwarbi;
36
Igali mwana wa Nathani kutoka Soba; Bani, Mgadi;
37
Seleki, Mwamoni; Naharai, Mbeerothi, aliyekuwa mbeba silaha za Yoabu mwana wa Seruya;
38
Ira, Mwithiri; Garebu, Mwithiri;
39
na Uria, Mhiti. Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options