Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Afflictions of the Wicked

95 mistari · 20 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa hiyo Bwana Mungu wake akamtia mikononi mwa mfalme wa Aramu. Waaramu wakamshinda, wakachukua watu wake wengi mateka na kuwaleta mpaka Dameski. Tena alitiwa mikononi mwa mfalme wa Israeli, ambaye aliwaua watu wake wengi.

  2. Kwa siku moja Peka mwana wa Remalia aliwaua askari 120,000 katika Yuda, kwa kuwa Yuda walikuwa wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao.

  3. Zikri, askari shujaa Mwefraimu, akamuua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu mkuu wa jumba la kifalme na Elikana aliyekuwa wa pili kwa mfalme.

  4. Waisraeli wakawachukua mateka kutoka ndugu zao, watu wapatao 200,000 hawa wakiwa ni wanawake, watoto wa kiume na wa kike. Wakachukua pia kiasi kikubwa cha nyara, ambazo walirudi nazo Samaria.

  5. Katika wakati wake wa mateso Mfalme Ahazi akazidi kukosa uaminifu kwa Bwana.

  6. “Lakini mara walipokuwa na raha, wakafanya maovu tena machoni pako. Kisha ukawaacha mikononi mwa adui zao, nao wakawatawala. Walipokulilia tena, ukasikia kutoka mbinguni, na kwa huruma zako ukawaokoa kila mara.

  7. “Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza.

  8. Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso, miaka yote aliwekewa mkorofi.

  9. Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu; humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita,

  10. “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake,

  11. ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake.

  12. Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.

  13. Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.

  14. Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.

  15. Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi.

  16. Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.

  17. “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? Ni mara ngapi maafa huwajia, yale yawapatayo ambayo Mungu huwapangia katika hasira yake?

  18. Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa Bwana unamzunguka mtu anayemtumaini.

  19. bali Bwana huwacheka waovu, kwa sababu anajua siku yao inakuja.

  20. Mungu anayemiliki milele, atawasikia na kuwaadhibu, watu ambao hawabadilishi njia zao, wala hawana hofu ya Mungu.

  21. Bali Mungu atawapiga kwa mishale, nao ghafula wataangushwa.

  22. Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao na kuwaleta kwenye maangamizi; wote wawaonao watatikisa vichwa vyao kwa dharau.

  23. Wanadamu wote wataogopa, watatangaza kazi za Mungu na kutafakari yale aliyoyatenda.

  24. Kwa hiyo watu wao huwageukia na kunywa maji tele.

  25. Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho!