Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Prayer Under Affliction

49 mistari · 17 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Tega sikio, Ee Bwana, usikie; fungua macho yako, Ee Bwana, uone; sikiliza maneno ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

  2. Sasa basi, Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, Ee Bwana, ndiwe Mungu.”

  3. Ee Mungu wetu, je, wewe hutawahukumu? Kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa linalokuja kutushambulia. Sisi hatujui la kufanya, bali macho yetu yanakutazama wewe.”

  4. “Basi sasa, Ee Mungu wetu, uliye mkuu, mwenye nguvu na Mungu wa kuogofya, mwenye kushika agano lake la upendo, usiache taabu hizi zote zionekane kuwa kitu kidogo mbele za macho yako, taabu hizi zilizotupata, juu ya wafalme wetu na viongozi, juu ya makuhani wetu na manabii, juu ya baba zetu na watu wako wote, tangu siku za wafalme wa Ashuru hadi leo.

  5. “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya; nionyesheni nilikokosea.

  6. Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.

  7. Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.

  8. Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako?

  9. Nifundishe nisichoweza kuona; kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’

  10. Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonyesha jema lolote?” Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako.

  11. Unirehemu Bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee Bwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali.

  12. Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

  13. Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida?

  14. Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

  15. kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

  16. Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu.

  17. Ee Mungu, wakomboe Israeli, katika shida zao zote!

  18. Nifundishe njia yako, Ee Bwana, niongoze katika njia iliyonyooka kwa sababu ya watesi wangu.

  19. “Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu na hesabu ya siku zangu; nijalie kujua jinsi maisha yangu yanavyopita upesi.

  20. Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.

  21. Niondolee mjeledi wako, nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako.

  22. “Ee Bwana, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote,

  23. Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena kabla sijaondoka na nisiwepo tena.”

  24. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba. Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu.

  25. Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi.