Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Miracles Wrought Through Servants of God

158 mistari · 74 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. hivi kwamba leso au vitambaa vilivyokuwa vimegusa mwili wa Paulo viliwekwa juu ya wagonjwa, nao wakapona magonjwa yao, na pepo wachafu wakawatoka.

  2. Paulo akashuka chini, akajitupa juu yake na kumkumbatia, akasema, “Msishtuke, uzima wake bado umo ndani yake.”

  3. Kisha Paulo akapanda tena ghorofani, akamega mkate na kula. Baada ya kuongea mpaka mapambazuko, akaondoka.

  4. Watu wakamrudisha yule kijana nyumbani akiwa hai nao wakafarijika sana.

  5. Lakini Paulo akamkungʼutia yule nyoka ndani ya moto wala yeye hakupata madhara yoyote.

  6. Baba yake Publio alikuwa mgonjwa kitandani, akiwa anaumwa homa na kuhara damu. Paulo akaingia ndani ili kumwona na baada ya maombi, akaweka mikono juu yake na kumponya.

  7. Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi. Akaomba kwa bidii kwamba mvua isinyeshe, nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.

  8. Kisha akaomba tena, nazo mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa mazao yake.