Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 7:5takriban 1490 KK

    “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”

  2. Hesabu 7:6takriban 1490 KK

    Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi.

  3. Hesabu 7:7takriban 1490 KK

    Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao,

  4. Hesabu 7:8takriban 1490 KK

    na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.

  5. Hesabu 7:9takriban 1490 KK

    Lakini Mose hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.

  6. Hesabu 7:10takriban 1490 KK

    Wakati madhabahu yalitiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu.

  7. Hesabu 7:11takriban 1490 KK

    Kwa maana Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”

  8. Hesabu 7:12takriban 1490 KK

    Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.

  9. Hesabu 7:13takriban 1490 KK

    Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

  10. Hesabu 7:14takriban 1490 KK

    sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

  11. Hesabu 7:15takriban 1490 KK

    fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

  12. Hesabu 7:16takriban 1490 KK

    mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

  13. Hesabu 7:17takriban 1490 KK

    maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.

  14. Hesabu 7:18takriban 1490 KK

    Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake.

  15. Hesabu 7:19takriban 1490 KK

    Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

  16. Hesabu 7:20takriban 1490 KK

    sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

  17. Hesabu 7:21takriban 1490 KK

    fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

  18. Hesabu 7:22takriban 1490 KK

    mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

  19. Hesabu 7:23takriban 1490 KK

    maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.

  20. Hesabu 7:24takriban 1490 KK

    Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake.

  21. Hesabu 7:25takriban 1490 KK

    Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

  22. Hesabu 7:26takriban 1490 KK

    sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

  23. Hesabu 7:27takriban 1490 KK

    fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

  24. Hesabu 7:28takriban 1490 KK

    mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

  25. Hesabu 7:29takriban 1490 KK

    maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.