Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Luka 21:19takriban 33 BK

    Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.

  2. Luka 21:20takriban 33 BK

    “Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi fahamuni kwamba kuharibiwa kwake kumekaribia.

  3. Luka 21:21takriban 33 BK

    Wakati huo, wale walio Uyahudi wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo, nao wale walioko mashambani wasiingie mjini.

  4. Luka 21:22takriban 33 BK

    Kwa sababu huu utakuwa ni wakati wa adhabu ili kutimiza yote yaliyoandikwa.

  5. Luka 21:23takriban 33 BK

    Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu.

  6. Luka 21:24takriban 33 BK

    Wataanguka kwa makali ya upanga, na wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote. Nao mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa Mataifa hadi muda wa hao watu wa Mataifa utimie.

  7. Luka 21:25takriban 33 BK

    “Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa kutokana na ngurumo na misukosuko ya bahari.

  8. Luka 21:26takriban 33 BK

    Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za angani zitatikisika.

  9. Luka 21:27takriban 33 BK

    Wakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu.

  10. Luka 21:28takriban 33 BK

    Mambo haya yatakapoanza kutendeka, simameni na mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umekaribia.”

  11. Luka 21:29takriban 33 BK

    Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote.

  12. Luka 21:30takriban 33 BK

    Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia.

  13. Luka 21:31takriban 33 BK

    Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.

  14. Luka 21:32takriban 33 BK

    “Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia.

  15. Luka 21:33takriban 33 BK

    Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”

  16. Luka 21:34takriban 33 BK

    “Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama vile mtego unasavyo.

  17. Luka 21:35takriban 33 BK

    Kwa maana kama vile mtego unasavyo, ndivyo siku hiyo itakavyowapata wanadamu wote waishio katika uso wa dunia yote.

  18. Luka 21:36takriban 33 BK

    Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.”

  19. Luka 21:37takriban 33 BK

    Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni, na jioni ilipofika, alikwenda zake kwenye Mlima wa Mizeituni na kukaa huko usiku kucha.

  20. Luka 21:38takriban 33 BK

    Nao watu wote walikuja asubuhi na mapema Hekaluni ili kumsikiliza.

  21. Luka 22:1takriban 33 BK

    Wakati huu Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia.

  22. Luka 22:2takriban 33 BK

    Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wanatafuta njia ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu.

  23. Luka 22:3takriban 33 BK

    Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili.

  24. Luka 22:4takriban 33 BK

    Yuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa maafisa wa walinzi wa Hekalu, akazungumza nao jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu.

  25. Luka 22:5takriban 33 BK

    Wakafurahi na wakakubaliana kumpa fedha.