Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Luka 20:41takriban 33 BK

    Kisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristoni Mwana wa Daudi?

  2. Luka 20:42takriban 33 BK

    Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume,

  3. Luka 20:43takriban 33 BK

    hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’

  4. Luka 20:44takriban 33 BK

    Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”

  5. Luka 20:45takriban 33 BK

    Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake,

  6. Luka 20:46takriban 33 BK

    “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu.

  7. Luka 20:47takriban 33 BK

    Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”

  8. Luka 21:1takriban 33 BK

    Yesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu.

  9. Luka 21:2takriban 33 BK

    Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba.

  10. Luka 21:3takriban 33 BK

    Yesu akasema, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote.

  11. Luka 21:4takriban 33 BK

    Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.”

  12. Luka 21:5takriban 33 BK

    Baadhi ya wanafunzi wake wakawa wanamwonyesha jinsi Hekalu lilivyopambwa kwa mawe mazuri na kwa vitu vilivyotolewa kuwa sadaka kwa Mungu. Lakini Yesu akawaambia,

  13. Luka 21:6takriban 33 BK

    “Kuhusu haya mnayoyaona hapa, wakati utafika ambapo hakuna jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”

  14. Luka 21:7takriban 33 BK

    Wakamuuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatukia lini? Ni dalili gani itaonyesha kwamba yanakaribia kutendeka?”

  15. Luka 21:8takriban 33 BK

    Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate.

  16. Luka 21:9takriban 33 BK

    Lakini msikiapo habari za vita na machafuko, msiogope. Kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila ule mwisho hautakuja wakati huo.”

  17. Luka 21:10takriban 33 BK

    Kisha akawaambia: “Taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme mmoja dhidi ya ufalme mwingine.

  18. Luka 21:11takriban 33 BK

    Kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, na njaa kali, na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali. Pia kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.

  19. Luka 21:12takriban 33 BK

    “Lakini kabla yote hayajatokea, watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawatia mikononi mwa wakuu wa masinagogi na kuwafunga magerezani. Nanyi mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya Jina langu.

  20. Luka 21:13takriban 33 BK

    Hii itawapa nafasi ya kushuhudia.

  21. Luka 21:14takriban 33 BK

    Lakini kusudieni mioyoni mwenu msisumbuke awali kuhusu mtakalosema mbele ya mashtaka.

  22. Luka 21:15takriban 33 BK

    Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo hakuna hata adui yenu mmoja atakayeweza kushindana nayo wala kuipinga.

  23. Luka 21:16takriban 33 BK

    Mtasalitiwa hata na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki, na baadhi yenu watawaua.

  24. Luka 21:17takriban 33 BK

    Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu.

  25. Luka 21:18takriban 33 BK

    Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia.