Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Isaya 23:3takriban 715 KK

    Kwenye maji makuu nafaka za Shihori zilikuja; mavuno ya Naili yalikuwa mapato ya Tiro, naye akawa soko la mataifa.

  2. Isaya 23:4takriban 715 KK

    Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari, kwa kuwa bahari imesema: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa, wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.”

  3. Isaya 23:5takriban 715 KK

    Habari ifikapo Misri, watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro.

  4. Isaya 23:6takriban 715 KK

    Vukeni mpaka Tarshishi, ombolezeni, enyi watu wa kisiwani.

  5. Isaya 23:7takriban 715 KK

    Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe, mji wa zamani, zamani kabisa ambao miguu yake imeuchukua kufanya makao nchi za mbali sana?

  6. Isaya 23:8takriban 715 KK

    Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia?

  7. Isaya 23:9takriban 715 KK

    Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye alipanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekesha wale wote ambao ni mashuhuri duniani.

  8. Isaya 23:10takriban 715 KK

    Ee Binti Tarshishi, pita katika nchi yako kama vile Mto Naili kwa kuwa huna tena bandari.

  9. Isaya 23:11takriban 715 KK

    Bwana amenyoosha mkono wake juu ya bahari na kuzifanya falme zake zitetemeke. Ametoa amri kuhusu Kanaani kwamba ngome zake ziangamizwe.

  10. Isaya 23:12takriban 715 KK

    Alisema, “Usizidi kufurahi, ee Bikira Binti Sidoni, sasa umepondwa! “Simama, vuka uende Kitimu; hata huko hutapata pumziko.”

  11. Isaya 23:13takriban 715 KK

    Tazama katika nchi ya Wakaldayo, watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo! Waashuru wameifanya nchi hiyo kuwa mahali pa viumbe wa jangwani. Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka, wameziteka ngome zake na kuziacha tupu na kuufanya kuwa magofu.

  12. Isaya 23:14takriban 715 KK

    Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi; ngome yenu imeangamizwa!

  13. Isaya 23:15takriban 715 KK

    Wakati huo Tiro utasahauliwa kwa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Lakini mwisho wa miaka hiyo sabini, itakuwa kwa Tiro kama ilivyo katika wimbo wa kahaba:

  14. Isaya 23:16takriban 715 KK

    “Twaa kinubi, tembea mjini kote, ewe kahaba uliyesahauliwa; piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi, ili upate kukumbukwa.”

  15. Isaya 23:17takriban 715 KK

    Mwishoni mwa miaka sabini, Bwana atashughulika na Tiro. Naye atarudia ajira yake ya ukahaba, na atafanya biashara yake na falme zote juu ya uso wa dunia.

  16. Isaya 23:18takriban 715 KK

    Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa Bwana; hayatahifadhiwa wala kufichwa. Faida zake zitakwenda kwa wale wakaao mbele za Bwana kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.

  17. Isaya 24:1takriban 712 KK

    Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa na kuiharibu, naye atauharibu uso wake na kutawanya wakaao ndani yake:

  18. Isaya 24:2takriban 712 KK

    ndivyo itakavyokuwa kwa makuhani na kwa watu, kwa bwana na kwa mtumishi, kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike, kwa muuzaji na kwa mnunuzi, kwa mkopaji na kwa mkopeshaji, kwa mdaiwa na kwa mdai.

  19. Isaya 24:3takriban 712 KK

    Dunia itaharibiwa kabisa na kutekwa nyara kabisa. Bwana amesema neno hili.

  20. Isaya 24:4takriban 712 KK

    Dunia inakauka na kunyauka, dunia inanyongʼonyea na kunyauka, waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea.

  21. Isaya 24:5takriban 712 KK

    Dunia imetiwa unajisi na watu wake; wameacha kutii sheria, wamevunja amri na kuvunja agano la milele.

  22. Isaya 24:6takriban 712 KK

    Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia, watu wake lazima waichukue hatia yao. Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa, nao waliosalia ni wachache sana.

  23. Isaya 24:7takriban 712 KK

    Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka, watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.

  24. Isaya 24:8takriban 712 KK

    Furaha ya matoazi imekoma, kelele za wenye furaha zimekoma, shangwe za kinubi zimenyamaza.

  25. Isaya 24:9takriban 712 KK

    Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo, kileo ni kichungu kwa wanywaji wake.