Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Petro 1:7takriban 60 BK

    Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atadhihirishwa.

  2. 1 Petro 1:8takriban 60 BK

    Ingawa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka.

  3. 1 Petro 1:9takriban 60 BK

    Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.

  4. 1 Petro 1:10takriban 60 BK

    Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa,

  5. 1 Petro 1:11takriban 60 BK

    wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata.

  6. 1 Petro 1:12takriban 60 BK

    Walidhihirishiwa kwamba walikuwa hawajihudumii wao wenyewe, bali waliwahudumia ninyi, waliponena kuhusu mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiria ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanatamani kuyafahamu mambo haya.

  7. 1 Petro 1:13takriban 60 BK

    Kwa hiyo, tayarisheni nia zenu kwa kazi; mwe na kiasi, mkitumainia kikamilifu ile neema mtakayopewa Yesu Kristo atakapodhihirishwa.

  8. 1 Petro 1:14takriban 60 BK

    Kama watoto watiifu, msifuate tamaa zenu mbaya wakati mlipoishi kwa ujinga.

  9. 1 Petro 1:15takriban 60 BK

    Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi kuweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.

  10. 1 Petro 1:16takriban 60 BK

    Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”

  11. 1 Petro 1:17takriban 60 BK

    Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni.

  12. 1 Petro 1:18takriban 60 BK

    Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu,

  13. 1 Petro 1:19takriban 60 BK

    bali kwa damu ya thamani ya Kristo, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa.

  14. 1 Petro 1:20takriban 60 BK

    Yeye alichaguliwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu.

  15. 1 Petro 1:21takriban 60 BK

    Kupitia kwake mmemwamini Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mungu.

  16. 1 Petro 1:22takriban 60 BK

    Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.

  17. 1 Petro 1:23takriban 60 BK

    Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele.

  18. 1 Petro 1:24takriban 60 BK

    Maana, “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni; majani hunyauka na maua huanguka,

  19. 1 Petro 1:25takriban 60 BK

    lakini neno la Bwana ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.

  20. 1 Petro 2:1takriban 60 BK

    Kwa hiyo, wekeni mbali nanyi uovu wote na udanganyifu wote, unafiki, wivu na masingizio ya kila namna.

  21. 1 Petro 2:2takriban 60 BK

    Kama watoto wachanga, waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya kiroho yasiyochanganywa na kitu kingine chochote, ili kwa hayo mpate kukua katika wokovu,

  22. 1 Petro 2:3takriban 60 BK

    ikiwa kweli mmeonja ya kwamba Bwana ni mwema.

  23. 1 Petro 2:4takriban 60 BK

    Mnapokuja kwake, yeye aliye Jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kwake,

  24. 1 Petro 2:5takriban 60 BK

    ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mnajengwa kuwa nyumba ya kiroho, ili mpate kuwa ukuhani mtakatifu, mkitoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.

  25. 1 Petro 2:6takriban 60 BK

    Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, naweka katika Sayuni, jiwe la pembeni teule lenye thamani, na yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe.”