Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Wafilipi 4:14takriban 64 BK

    Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu.

  2. Wafilipi 4:15takriban 64 BK

    Zaidi ya hayo, ninyi Wafilipi mnajua kwamba siku za kwanza nilipoanza kuhubiri Injili, nilipoondoka Makedonia, hakuna kanisa jingine lililoshiriki nami katika masuala ya kutoa na kupokea isipokuwa ninyi.

  3. Wafilipi 4:16takriban 64 BK

    Kwa maana hata nilipokuwa huko Thesalonike, mliniletea msaada kwa ajili ya mahitaji yangu zaidi ya mara moja.

  4. Wafilipi 4:17takriban 64 BK

    Si kwamba natafuta sana yale matoleo, bali natafuta sana ile faida itakayozidi sana kwa upande wenu.

  5. Wafilipi 4:18takriban 64 BK

    Nimelipwa kikamilifu hata na zaidi; nimetoshelezwa kabisa sasa, kwa kuwa nimepokea kutoka kwa Epafrodito vile vitu mlivyonitumia, sadaka yenye harufu nzuri, dhabihu inayokubalika na ya kumpendeza Mungu.

  6. Wafilipi 4:19takriban 64 BK

    Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu.

  7. Wafilipi 4:20takriban 64 BK

    Mungu wetu aliye Baba yetu apewe utukufu milele na milele. Amen.

  8. Wafilipi 4:21takriban 64 BK

    Msalimuni kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walioko pamoja nami wanawasalimu.

  9. Wafilipi 4:22takriban 64 BK

    Watakatifu wote wanawasalimu, hasa wale watu wa nyumbani mwa Kaisari.

  10. Wafilipi 4:23takriban 64 BK

    Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.

  11. Wakolosai 1:1takriban 64 BK

    Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu:

  12. Wakolosai 1:2takriban 64 BK

    Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, waishio Kolosai: Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu ziwe nanyi.

  13. Wakolosai 1:3takriban 64 BK

    Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi,

  14. Wakolosai 1:4takriban 64 BK

    kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote:

  15. Wakolosai 1:5takriban 64 BK

    imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili

  16. Wakolosai 1:6takriban 64 BK

    iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote.

  17. Wakolosai 1:7takriban 64 BK

    Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu,

  18. Wakolosai 1:8takriban 64 BK

    ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho.

  19. Wakolosai 1:9takriban 64 BK

    Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu.

  20. Wakolosai 1:10takriban 64 BK

    Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu,

  21. Wakolosai 1:11takriban 64 BK

    mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha

  22. Wakolosai 1:12takriban 64 BK

    mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru.

  23. Wakolosai 1:13takriban 64 BK

    Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa,

  24. Wakolosai 1:14takriban 64 BK

    ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.

  25. Wakolosai 1:15takriban 64 BK

    Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.