Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Wicked

724 mistari · 18 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.

  2. Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi.

  3. Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.

  4. Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu; amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga.

  5. “Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana; hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.

  6. Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; kufanikiwa kwake hakutadumu.

  7. Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote.

  8. Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake.

  9. Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma.

  10. Atauchomoa katika mgongo wake, ncha ingʼaayo kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake;

  11. giza nene linavizia hazina zake. Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.

  12. Mbingu zitaweka wazi hatia yake, nayo nchi itainuka kinyume chake.

  13. Mafuriko yataichukua nyumba yake, maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.

  14. Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”

  15. Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu?

  16. Huwaona watoto wao wakithibitika wakiwa wamewazunguka, wazao wao mbele za macho yao.

  17. Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; fimbo ya Mungu haiko juu yao.

  18. Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe; ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba.

  19. Huwatoa watoto wao nje kama kundi; wadogo wao huchezacheza.

  20. Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, nao huifurahia sauti ya filimbi.

  21. Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani.

  22. Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako.

  23. Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba?

  24. Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe, hivyo najitenga mbali na shauri la waovu.

  25. “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? Ni mara ngapi maafa huwajia, yale yawapatayo ambayo Mungu huwapangia katika hasira yake?