Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Music

324 mistari · 57 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana,

  2. ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.

  3. Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.

  4. Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni.

  5. Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu,

  6. kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!”

  7. Tutaimbaje nyimbo za Bwana, tukiwa nchi ya kigeni?

  8. Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.

  9. Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa.

  10. Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,

  11. Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

  12. Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.

  13. Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

  14. Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,

  15. Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu.

  16. Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

  17. Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze,

  18. msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

  19. msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

  20. Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!

  21. Kama vile avuaye mavazi siku ya baridi, au kama siki iliyomwagwa juu ya magadi, ndivyo alivyo yeye amuimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.

  22. Nikajikusanyia fedha na dhahabu, hazina za wafalme na za majimbo. Nikajipatia waimbaji wanaume na wanawake, nazo nyumba za masuria: vitu ambavyo moyo wa mwanadamu hufurahia.

  23. Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani, hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu. Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote, hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote.

  24. Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo mikono yangu ilikuwa imefanya na yale niliyotaabika kukamilisha, kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbiza upepo; hapakuwa na faida yoyote chini ya jua.

  25. Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao, matari, filimbi na mvinyo, lakini hawayajali matendo ya Bwana, wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake.