Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Miracles

338 mistari · 37 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa makusudi walimjaribu Mungu, wakidai vyakula walivyovitamani.

  2. Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani?

  3. Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, vijito vikatiririka maji mengi. Lakini je, aweza kutupa chakula pia? Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?”

  4. Bwana alipowasikia, alikasirika sana, moto wake ukawa dhidi ya Yakobo, na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli,

  5. kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake.

  6. Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu na kufungua milango ya mbingu,

  7. akawanyeshea mana ili watu wale; aliwapa nafaka ya mbinguni.

  8. Watu walikula mkate wa malaika, akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula.

  9. Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake.

  10. Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, ndege warukao kama mchanga wa pwani.

  11. Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, kuzunguka mahema yao yote.

  12. Walikula na kusaza, kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani.

  13. Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao,

  14. hasira ya Mungu ikawaka juu yao, akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, akiwaangusha vijana wa Israeli.

  15. Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini.

  16. Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,

  17. Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.

  18. Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.

  19. Aliwaokoa mikononi mwa adui; kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.

  20. Maji yaliwafunika adui zao, hakunusurika hata mmoja.

  21. Ndipo walipoamini ahadi zake, nao wakaimba sifa zake.

  22. Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa, kwa ajabu juu ya ajabu. Hekima ya wenye hekima itapotea, nayo akili ya wenye akili itatoweka.”

  23. Ulitenda ishara za miujiza na maajabu huko Misri, na umeyaendeleza mpaka leo, katika Israeli na miongoni mwa wanadamu wote, nawe umejulikana na kufahamika hivyo mpaka leo.

  24. Uliwatoa watu wako Israeli kutoka Misri kwa ishara na maajabu, kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa na kwa matisho makuu.

  25. Mfalme akamwambia Danieli, “Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, na mfunuaji wa siri zote, kwa maana umeweza kufunua siri hii.”