Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Jerusalem: Annual feasts kept at

17 mistari · 117 vipengele

Mistari kuhusu Annual feasts kept at

  1. Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja.

  2. Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli.

  3. Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

  4. Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumuua.

  5. Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.

  6. Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.

  7. Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jionyeshe kwa ulimwengu.”

  8. Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini.

  9. Yesu akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote.

  10. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu.

  11. Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.”

  12. Akiisha kusema hayo, akabaki Galilaya.

  13. Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri.

  14. Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?”

  15. Kulikuwa na minongʼono iliyoenea kumhusu Yesu katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”

  16. Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.

  17. Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.