Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Jerusalem: Disciples persecuted and dispersed from

7 mistari · 117 vipengele

Mistari kuhusu Disciples persecuted and dispersed from

  1. Naye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano. Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria.

  2. Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana.

  3. Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani.

  4. Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda.

  5. Basi wale waliotawanyika kwa ajili ya mateso yaliyotokana na kifo cha Stefano, wakasafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia. Nao hawakuhubiri lile Neno kwa mtu yeyote isipokuwa Wayahudi.

  6. Lakini baadhi yao walikuwepo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria habari njema za Bwana Yesu.

  7. Mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, nayo idadi kubwa ya watu wakaamini na kumgeukia Bwana.