Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Integrity

96 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake,

  2. ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia.

  3. Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika.

  4. Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

  5. Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.

  6. Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

  7. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Bwana bila kusitasita.

  8. Ee Bwana, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu;

  9. kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako.

  10. Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama.

  11. Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu.

  12. Wao hawana taabu, miili yao ina afya na nguvu.

  13. Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.

  14. Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri.

  15. Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi, majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo.

  16. Hudhihaki na kusema kwa ukorofi, katika majivuno yao wanatishia kutesa.

  17. Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu, nazo ndimi zao humiliki duniani.

  18. Kwa hiyo watu wao huwageukia na kunywa maji tele.

  19. Wanasema, “Mungu awezaje kujua? Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?”

  20. Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri.

  21. Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.

  22. Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi.

  23. Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.

  24. Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa.

  25. Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao.