Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Integrity

96 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu.

  2. Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho!

  3. Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto.

  4. Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu,

  5. nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.

  6. Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako.

  7. Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu.

  8. Macho yako na yatazame mbele, kaza macho yako moja kwa moja mbele yako.

  9. Sawazisha mapito ya miguu yako na njia zako zote ziwe zimethibitika.

  10. Usigeuke kulia wala kushoto; epusha mguu wako na ubaya.

  11. Yeye aendaye kwa uadilifu na kusema lililo haki, yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji, na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:

  12. huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu, ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani. Atapewa mkate wake, na maji yake hayatakoma.

  13. Hamwonei mtu yeyote, bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake. Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake na huwapa nguo walio uchi.

  14. Hakopeshi kwa riba wala hajipatii faida ya ziada. Huuzuia mkono wake usifanye mabaya, naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.

  15. Huzifuata amri zangu na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu. Huyo mtu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana Mwenyezi.

  16. Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.”

  17. Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”

  18. Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana.

  19. Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu,

  20. Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali.

  21. Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.