Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Enemy

57 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu, sawasawa na haki yako; usiwaache wakusimange.

  2. Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!” Au waseme, “Tumemmeza.”

  3. Wote wanaofurahia dhiki yangu waaibishwe na wachanganyikiwe; hao wanaojiinua dhidi yangu wavikwe aibu na dharau.

  4. Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “Bwana atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”

  5. Ulimi wangu utanena haki yako na sifa zako mchana kutwa.

  6. kwa maana watu waovu na wadanganyifu wamefungua vinywa vyao dhidi yangu; wasema dhidi yangu kwa ndimi za udanganyifu.

  7. Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, wananishambulia bila sababu.

  8. Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, lakini mimi ninawaombea.

  9. Wananilipiza mabaya kwa mema, chuki badala ya urafiki wangu.

  10. Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:

  11. wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.

  12. Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.

  13. Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie.

  14. Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.

  15. Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale; kama ana kiu, mpe maji anywe.

  16. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake, naye Bwana atakupa thawabu.

  17. “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’

  18. Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi,

  19. ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

  20. Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?

  21. Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo?

  22. Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

  23. “Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia.

  24. Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.

  25. Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyangʼanya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia.