Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Alliance and Society with the Enemies of God

229 mistari · 51 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!

  2. Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.

  3. Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!

  4. Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao.

  5. Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

  6. tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.

  7. Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara.

  8. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

  9. Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao,

  10. Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.

  11. Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda.

  12. Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,

  13. wale waachao mapito yaliyonyooka wakatembea katika njia za giza,

  14. wale wapendao kutenda mabaya na kufurahia upotovu wa ubaya,

  15. ambao mapito yao yamepotoka na ambao ni wapotovu katika njia zao.

  16. Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya,

  17. aliyemwacha mwenzi wa ujana wake na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.

  18. Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo na mapito yake kwenye roho za waliokufa.

  19. Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima.

  20. Hivyo utatembea katika njia za watu wema na kushikamana na mapito ya wenye haki.

  21. Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya watu wabaya.

  22. Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo; achana nayo, na uelekee njia yako.

  23. Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.

  24. Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.

  25. Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.