Mistari ya Biblia kuhusu Alliance and Society with the Enemies of God: Means of preservation from
Mistari kuhusu Means of preservation from
Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.
Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda.
Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,
wale waachao mapito yaliyonyooka wakatembea katika njia za giza,
wale wapendao kutenda mabaya na kufurahia upotovu wa ubaya,
ambao mapito yao yamepotoka na ambao ni wapotovu katika njia zao.
Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya,
aliyemwacha mwenzi wa ujana wake na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.
Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo na mapito yake kwenye roho za waliokufa.
Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima.
Hivyo utatembea katika njia za watu wema na kushikamana na mapito ya wenye haki.
Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.