Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Alliance and Society with the Enemies of God: Exhortations to shun all inducements to

9 mistari · 51 vipengele

Mistari kuhusu Exhortations to shun all inducements to

  1. Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao.

  2. Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

  3. tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.

  4. Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara.

  5. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

  6. Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao,

  7. Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya watu wabaya.

  8. Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo; achana nayo, na uelekee njia yako.

  9. Basi, ninyi wapenzi, kwa kuwa mmekwisha kujua mambo haya, jilindeni msije mkachukuliwa na kosa la watu hao waasi na kuanguka kutoka kwenye uthabiti wenu.