Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Afflictions Made Beneficial

104 mistari · 23 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

  2. “Kama mwanadamu akimwambia Mungu, ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena.

  3. Nifundishe nisichoweza kuona; kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’

  4. Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,

  5. huwaonyesha yale waliyoyatenda, kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.

  6. Kisha nilikujulisha dhambi yangu wala sikuficha uovu wangu. Nilisema, “Nitaungama makosa yangu kwa Bwana.” Ndipo uliponisamehe hatia ya dhambi yangu.

  7. Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,

  8. huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.

  9. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

  10. Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima.

  11. Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.

  12. Ee Mungu, wewe ulitujaribu, ukatusafisha kama fedha.

  13. Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku.

  14. Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.

  15. Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.

  16. Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali Bwana huujaribu moyo.

  17. Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu, kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu, imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao.

  18. Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo.

  19. Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu, nitawasafisha takataka zenu zote na kuwaondolea unajisi wenu wote.

  20. Nitawarudishia waamuzi wenu kama ilivyokuwa siku za zamani, nao washauri wenu kama ilivyokuwa mwanzoni. Baadaye utaitwa, Mji wa Haki, Mji Mwaminifu.”

  21. Katika siku ile, mabaki ya Israeli, walionusurika wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, lakini watamtegemea kwa kweli Bwana Aliye Mtakatifu wa Israeli.

  22. Mabaki watarudi, mabaki wa Yakobo watamrudia Mungu Mwenye Nguvu.

  23. Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku, wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku. Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia, watu wa ulimwengu hujifunza haki.

  24. Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha, nimekujaribu katika tanuru ya mateso.

  25. Unakaa katikati ya udanganyifu; katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,” asema Bwana.