Mistari ya Biblia kuhusu Afflictions Made Beneficial: In exhibiting the power and faithfulness of God
Mistari kuhusu In exhibiting the power and faithfulness of God
Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,
huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.
Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa;
twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.
Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Yesu ili kwamba uzima wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu.
Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti.