Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Nyakati 23:7takriban 1015 KK

    Wana wa Wagershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei.

  2. 1 Nyakati 23:8takriban 1015 KK

    Wana wa Ladani walikuwa watatu: Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.

  3. 1 Nyakati 23:9takriban 1015 KK

    Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomothi, Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.

  4. 1 Nyakati 23:10takriban 1015 KK

    Nao wana wa Shimei walikuwa wanne: Yahathi, Zina, Yeushi na Beria.

  5. 1 Nyakati 23:11takriban 1015 KK

    Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.

  6. 1 Nyakati 23:12takriban 1015 KK

    Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

  7. 1 Nyakati 23:13takriban 1015 KK

    Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele.

  8. 1 Nyakati 23:14takriban 1015 KK

    Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.

  9. 1 Nyakati 23:15takriban 1015 KK

    Wana wa Mose walikuwa: Gershomu na Eliezeri.

  10. 1 Nyakati 23:16takriban 1015 KK

    Wazao wa Gershomu: Shebueli alikuwa wa kwanza.

  11. 1 Nyakati 23:17takriban 1015 KK

    Wazao wa Eliezeri: Rehabia alikuwa wa kwanza. Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

  12. 1 Nyakati 23:18takriban 1015 KK

    Wana wa Ishari: Shelomithi alikuwa wa kwanza.

  13. 1 Nyakati 23:19takriban 1015 KK

    Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.

  14. 1 Nyakati 23:20takriban 1015 KK

    Wana wa Uzieli walikuwa: Mika wa kwanza na Ishia wa pili.

  15. 1 Nyakati 23:21takriban 1015 KK

    Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Wana wa Mahli walikuwa: Eleazari na Kishi.

  16. 1 Nyakati 23:22takriban 1015 KK

    Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

  17. 1 Nyakati 23:23takriban 1015 KK

    Wana wa Mushi: Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.

  18. 1 Nyakati 23:24takriban 1015 KK

    Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la Bwana.

  19. 1 Nyakati 23:25takriban 1015 KK

    Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele,

  20. 1 Nyakati 23:26takriban 1015 KK

    Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.”

  21. 1 Nyakati 23:27takriban 1015 KK

    Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

  22. 1 Nyakati 23:28takriban 1015 KK

    Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.

  23. 1 Nyakati 23:29takriban 1015 KK

    Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa.

  24. 1 Nyakati 23:30takriban 1015 KK

    Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni

  25. 1 Nyakati 23:31takriban 1015 KK

    na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.