Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 20:28takriban 33 BK

    kama vile ambavyo Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”

  2. Mathayo 20:29takriban 33 BK

    Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu ulimfuata.

  3. Mathayo 20:30takriban 33 BK

    Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

  4. Mathayo 20:31takriban 33 BK

    Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie.”

  5. Mathayo 20:32takriban 33 BK

    Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”

  6. Mathayo 20:33takriban 33 BK

    Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.”

  7. Mathayo 20:34takriban 33 BK

    Yesu akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.

  8. Mathayo 21:1takriban 33 BK

    Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili,

  9. Mathayo 21:2takriban 33 BK

    akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee.

  10. Mathayo 21:3takriban 33 BK

    Kama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”

  11. Mathayo 21:4takriban 33 BK

    Haya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema:

  12. Mathayo 21:5takriban 33 BK

    “Mwambieni Binti Sayuni, ‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mnyenyekevu, naye amepanda punda, juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”

  13. Mathayo 21:6takriban 33 BK

    Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza.

  14. Mathayo 21:7takriban 33 BK

    Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake.

  15. Mathayo 21:8takriban 33 BK

    Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani.

  16. Mathayo 21:9takriban 33 BK

    Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema, “Hosana, Mwana wa Daudi!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Hosana juu mbinguni!”

  17. Mathayo 21:10takriban 33 BK

    Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?”

  18. Mathayo 21:11takriban 33 BK

    Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”

  19. Mathayo 21:12takriban 33 BK

    Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.

  20. Mathayo 21:13takriban 33 BK

    Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.”

  21. Mathayo 21:14takriban 33 BK

    Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya.

  22. Mathayo 21:15takriban 33 BK

    Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika.

  23. Mathayo 21:16takriban 33 BK

    Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa’?”

  24. Mathayo 21:17takriban 33 BK

    Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.

  25. Mathayo 21:18takriban 33 BK

    Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa.