Rukia maudhui

circa 1380–1050 BC

The Judges & Ruth

Israel cycles through rebellion, oppression, and rescue under charismatic leaders—culminating in Ruth's faithful love story.

703 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waamuzi 20:6takriban 1406 KK

    Ndipo nikamchukua suria wangu, nikamkatakata vipande vipande na kuvipeleka katika nchi yote ya urithi wa Israeli, kwa kuwa wametenda uasherati mkubwa na jambo la aibu katika Israeli.

  2. Waamuzi 20:7takriban 1406 KK

    Sasa, ninyi Waisraeli wote, semeni na mtoe uamuzi wenu.”

  3. Waamuzi 20:8takriban 1406 KK

    Watu wote wakainuka wakasema, kama mtu mmoja, “Hakuna hata mmoja wetu atakayekwenda nyumbani. Wala hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake.

  4. Waamuzi 20:9takriban 1406 KK

    Sasa hili ndilo tutakaloitendea Gibea: Tutaikabili jinsi kura itakavyotuongoza.

  5. Waamuzi 20:10takriban 1406 KK

    Tutatoa watu kumi katika kila 100 kutoka kwenye kabila zote za Israeli, watu 100 katika watu 1,000 na watu 1,000 katika 10,000, ili waende wakalete mahitaji kwa ajili ya jeshi. Basi wakati jeshi litakapofika Gibea ya Benyamini, watawatendea yale wanayostahili, kwa ajili ya uovu huu wa aibu waliotenda katika Israeli.”

  6. Waamuzi 20:11takriban 1406 KK

    Hivyo wanaume wote wa Israeli wakakutanika pamoja na kujiunga kama mtu mmoja dhidi ya huo mji.

  7. Waamuzi 20:12takriban 1406 KK

    Makabila ya Israeli yakatuma watu kwenda katika kabila la Benyamini lote na kuwaambia, “Ni uovu gani huu wa kutisha uliotendeka katikati yenu?

  8. Waamuzi 20:13takriban 1406 KK

    Basi watoeni hao watu waovu kabisa walioko Gibea, ili tupate kuwaua na kuondoa uovu katika Israeli.” Lakini Wabenyamini hawakuwasikia ndugu zao, Waisraeli.

  9. Waamuzi 20:14takriban 1406 KK

    Wakatoka katika miji yao, wakakutanika Gibea ili kupigana na Waisraeli.

  10. Waamuzi 20:15takriban 1406 KK

    Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu 26,000 kutoka miji yao, waliojifunga panga, mbali na hao 700 waliochaguliwa miongoni mwa hao waliokaa Gibea.

  11. Waamuzi 20:16takriban 1406 KK

    Miongoni mwa hao askari wote kulikuwa na watu 700 bora waliochaguliwa watumiao mkono wa kushoto, kila mmoja wao aliweza kutupa jiwe kwa kombeo na kulenga unywele mmoja bila kukosa.

  12. Waamuzi 20:17takriban 1406 KK

    Nao watu wa Israeli, mbali na hao wa Benyamini, wakakusanya watu waume 400,000, wenye kutumia panga, wote hao walikuwa mashujaa.

  13. Waamuzi 20:18takriban 1406 KK

    Waisraeli wakapanda Betheli na kumuuliza Mungu, “Ni nani miongoni mwetu atakayetangulia mbele yetu ili kupigana na Wabenyamini?” Bwana akawajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia.”

  14. Waamuzi 20:19takriban 1406 KK

    Asubuhi yake Waisraeli wakaamka na kupiga kambi karibu na Gibea.

  15. Waamuzi 20:20takriban 1406 KK

    Waisraeli wakatoka kupigana na Wabenyamini, nao Waisraeli wakajiweka kwenye nafasi zao katika vita dhidi yao huko Gibea.

  16. Waamuzi 20:21takriban 1406 KK

    Wabenyamini wakatoka Gibea na kuwaua watu 22,000 wa Israeli siku ile.

  17. Waamuzi 20:22takriban 1406 KK

    Lakini Waisraeli wakatiana moyo kila mmoja na mwenzake, nao wakajiweka kwenye nafasi zao katika vile vita mara ya pili mahali pale walipokuwa wamejiweka mara ya kwanza.

  18. Waamuzi 20:23takriban 1406 KK

    Waisraeli wakapanda mbele za Bwana na kulia mbele zake mpaka jioni, nao wakamuuliza Bwana wakisema, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?” Bwana akajibu, “Pandeni mkapigane nao.”

  19. Waamuzi 20:24takriban 1406 KK

    Ndipo Waisraeli wakawakaribia Wabenyamini siku ya pili.

  20. Waamuzi 20:25takriban 1406 KK

    Wakati huu, Wabenyamini walipotoka Gibea ili kupigana nao, wakawaua watu Waisraeli 18,000, wote wakiwa wamejifunga panga.

  21. Waamuzi 20:26takriban 1406 KK

    Ndipo Waisraeli, watu wote, wakapanda Betheli, huko wakakaa mbele za Bwana wakilia. Wakafunga siku ile mpaka jioni na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani kwa Bwana.

  22. Waamuzi 20:27takriban 1406 KK

    Nao Waisraeli wakauliza kwa Bwana. (Katika siku hizo Sanduku la Agano la Mungu lilikuwa huko

  23. Waamuzi 20:28takriban 1406 KK

    na Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Aroni, alikuwa anahudumu mbele za hilo Sanduku.) Wakauliza, “Je, tupande kwenda vitani kupigana tena na Wabenyamini ndugu zetu, au la?” Bwana akajibu, “Nendeni, kwa kuwa kesho nitawatia mikononi mwenu.”

  24. Waamuzi 20:29takriban 1406 KK

    Basi Waisraeli wakaweka waviziao kuizunguka Gibea.

  25. Waamuzi 20:30takriban 1406 KK

    Kisha Waisraeli wakapanda kupigana na Wabenyamini katika siku ya tatu na kujiweka kwenye nafasi zao dhidi ya Gibea kama walivyokuwa wamefanya hapo kwanza.