Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’ ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo.

  2. Laiti ningefahamu mahali pa kumwona; laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!

  3. Ningeliweka shauri langu mbele zake, na kukijaza kinywa changu na hoja.

  4. Ningejua kwamba angenijibu nini, na kuelewa lile ambalo angelisema.

  5. Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? La, asingenigandamiza.

  6. Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.

  7. “Lakini nikienda mashariki, hayupo; nikienda magharibi, simpati.

  8. Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.

  9. Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

  10. Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu; nimeishika njia yake bila kukengeuka.

  11. Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.

  12. “Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? Yeye hufanya lolote atakalo.

  13. Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.

  14. Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake; nifikiriapo haya yote ninamwogopa.

  15. Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; yeye Mwenyezi amenitia hofu.

  16. Hata hivyo sijanyamazishwa na giza, wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.

  17. “Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio?

  18. Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote kwa kutenda mabaya.

  19. Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, lakini macho yake yanaona njia zao.

  20. “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

  21. Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

  22. Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

  23. Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake,

  24. Mauti iko wazi mbele za Mungu; Uharibifu haukufunikwa.

  25. Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.