Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Huufunika uso wa mwezi mpevu, akitandaza mawingu juu yake.

  2. Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea.

  3. Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande.

  4. Aliisafisha anga kwa pumzi yake; kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

  5. Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?”

  6. “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu, Mwenyezi ambaye amenifanya nionje uchungu wa nafsi,

  7. kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,

  8. Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; hadi nife, sitakana uadilifu wangu.

  9. Kwa maana mtu asiyemcha Mungu analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, Mungu anapouondoa uhai wake?

  10. Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?

  11. Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? Je, atamwita Mungu nyakati zote?

  12. “Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; njia za Mwenyezi sitazificha.

  13. “Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:

  14. Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.

  15. Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima.

  16. Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; macho yake huona hazina zake zote.

  17. Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.

  18. Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,

  19. kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia na huona kila kitu chini ya mbingu.

  20. Alipofanyiza nguvu za upepo na kuyapima maji,

  21. alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia kwa ajili ya umeme wa radi,

  22. ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, akaithibitisha na kuihakikisha.

  23. Naye Mungu akamwambia mwanadamu, ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

  24. “Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda,

  25. wakati taa yake iliniangazia kichwani changu, na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza!