Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.

  2. Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake.

  3. Mafuriko yataichukua nyumba yake, maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.

  4. Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”

  5. Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; fimbo ya Mungu haiko juu yao.

  6. Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako.

  7. Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba?

  8. “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? Ni mara ngapi maafa huwajia, yale yawapatayo ambayo Mungu huwapangia katika hasira yake?

  9. Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu kwa ajili ya wanawe.’ Mungu na amlipe mtu mwenyewe, ili apate kulijua!

  10. Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake; yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi.

  11. “Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa, iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote?

  12. “Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi?

  13. Je, Mwenyezi angefurahia nini kama ungekuwa mwadilifu? Au je, yeye angepata faida gani kama njia zako zingekuwa kamilifu?

  14. “Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea na kuleta mashtaka dhidi yako?

  15. “Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu? Juu kuliko nyota zilizo juu sana!

  16. Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’ Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo?

  17. Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi atembeapo juu ya anga la dunia.

  18. Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi! Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’

  19. Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri, hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu.

  20. “Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndipo mema yatakapokujia.

  21. Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake, na maneno yake uyaweke moyoni mwako.

  22. Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako,

  23. ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora.

  24. Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako.

  25. Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako.