Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.

  2. Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi.

  3. Kwake kuna nguvu na ushindi; adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.

  4. Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.

  5. Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga; huwafanya wapepesuke kama walevi.

  6. Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.

  7. Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?

  8. Mtamwonyesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?

  9. Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?

  10. Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?

  11. Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.

  12. Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu atakayethubutu kuja mbele yake!

  13. “Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, nami sitajificha uso wako:

  14. Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.

  15. Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu.

  16. Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako?

  17. Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?

  18. Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.

  19. Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.

  20. Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? Je, utamleta mbele yako katika hukumu?

  21. Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka; umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka.

  22. “Laiti kama ungenificha kaburini, na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka!

  23. Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.

  24. Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, lakini hutazifuatia dhambi zangu.

  25. Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko, nawe utazifunika dhambi zangu.