Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe.

  2. anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo,

  3. ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi,

  4. kumwonea huruma na kusema, ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; nimepata ukombozi kwa ajili yake’:

  5. Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.

  6. “Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; mara mbili hata mara tatu,

  7. “Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, lakini Mungu ameninyima haki yangu.

  8. Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote anapojitahidi kumpendeza Mungu.’

  9. “Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu. Kamwe Mungu hatendi uovu, Mwenyezi hafanyi kosa.

  10. Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda; huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili.

  11. Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa, kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu.

  12. Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia? Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote?

  13. Kama lilikuwa kusudi la Mungu, naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake,

  14. Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala? Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote?

  15. yeye asiyependelea wakuu, wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake?

  16. “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao.

  17. Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana, ili apate kuja mbele zake kwa hukumu.

  18. Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote, huwaondoa usiku, nao wakaangamia.

  19. kwa sababu wameacha kumfuata Mungu, nao hawakuiheshimu njia yake hata moja.

  20. Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake, hivyo akasikia kilio cha wahitaji.

  21. Lakini kama akinyamaza kimya, ni nani awezaye kumhukumu? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumwona? Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa,

  22. “Kama mwanadamu akimwambia Mungu, ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena.

  23. Nifundishe nisichoweza kuona; kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’

  24. Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako, wakati wewe umekataa kutubu? Yakupasa wewe uamue, wala si mimi; sasa niambie lile ulijualo.

  25. Kwenye dhambi yake huongeza uasi; kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu, na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”