God
Mistari inayomtaja God
Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi, na kuuagiza kulenga shabaha yake.
Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake.
Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote na kuupeleka hata miisho ya dunia.
Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake ingurumapo tena, huuachilia umeme wake wa radi.
Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu; yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.
Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’
Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.
Pumzi ya Mungu hutoa barafu, eneo kubwa la maji huganda.
Huyasheheneza mawingu kwa maji, naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.
Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, juu ya uso wa dunia yote, kufanya lolote ayaamuruyo.
Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu, au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.
“Ayubu, sikiliza hili; nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu.
Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu, na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga?
Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia, hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa?
Wewe unayeshindwa na joto katika nguo zako wakati nchi imenyamazishwa kimya bila upepo wa kusini,
je, waweza kuungana naye katika kuzitandaza anga, zilizo ngumu kama kioo cha shaba ya kuyeyushwa?
“Tuambieni yatupasayo kumwambia; hatuwezi kutayarisha shauri letu kwa sababu ya ujinga wetu.
Je, aambiwe kwamba nataka kuongea? Je, yuko mtu ambaye angeomba kumezwa?
Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu; Mungu huja katika utukufu wa kutisha.
Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza; katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea.
Kwa hiyo, wanadamu mheshimuni, kwa kuwa yeye hamstahi yeyote anayejidhania kuwa ana hekima.”
Kisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:
Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza swali, nawe unijibu.
“Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu.
wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?